Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro.
Waziri huyo pia amewataka watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo kuvunjwa.
Amesema hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze tusiwakwamishe.
Amesema wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na kudai Januari mosi ataenda tena kukagua kuona kama agizo lake limefanyiwa kazi.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema wamelisikia agizo la Waziri na wataenda kulitekeleza kama lilivyo.