Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu na Jokae Mwegelo wameteuliwa kuwa wajumbe kwa mwaka huu katika wizara ya maliasili ili wawezi kuwa mabalozi katika swala la utunzaji wa mali ya asili ikiwa ni mwezi wa maadhimisho ya Urithi wa maliasili Tanzania.
Mapema jana waziri wa maliasili Mh. Kigwangala aliteua mabalozi nane watakao kuwepo katika kamati ya maalumu ya taifa itakayohusika na maandalizi ya maadhimisho ya utunzaji wa maliasili tanzania ambapo Wema Sepetu na Jokate Mwegelo watakuwepo kaatika kamati hiyo.
Taarifa ya uteuzi ilisema kuwa imeongeza majina ya wajumbe wa kamati ya utunzaji wa urithi tanzania, ilikupata wawakilishi wa watu wa zanzibar na viajana pia, kamati hiyo itahusika na kuweka sawa wazo hili nakuweka swa mambo yote.
Haijawai kusemwa hadharani kama wawili hao walishawai kuwa maadui lakini mashabiki wanapata tumaini kubwa kuwa wawili hao watakapofanya kazi pamoja basi kila kitu kitakuwa sawa tena hasa ukizingatia wawili hao wamekuwa ni watu wenye nafasi kubwa sana katika jamii hasa katika maswala ya uhamasishaji.