Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dudu Baya ameiomba Serikali kupitia BASATA kuwachukulia hatua wasanii wote ambao wameenda kinyume na maadali kwa mwaka 2017.

Duba Baya amesema kuwa baadhi ya wasanii mwaka huu wameitumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuweka picha zisizo na maadili kitu ambacho kimefanya jambo hilo kujadiliwa kuliko muziki wao.

Dudu Baya amsema kuwa ”Watu kama kina Nuh Mziwanda wanapiga picha za uchi uko na Shilole kipindi kile uko bafuni unaoga kuna aja gani kuonyesha mashabiki wako, kuna mtu gani asiyeoga hapa duniani. Ukija kama suala la mdogo wangu Young Dee namkubali sana lakini alipiga picha na Amber Lulu za kumshika makalio, huo ni ujinga,” amesema Dudu Baya.

Dudu Baya ameendelea kwa kusema wasanii watumie mitandao kwa manufaa ya kibiashara na endapo wakishindwa basi sheria ichukue mkondo wake.

Ameendelea kusema kuwa “Nabahatika nakutana na Amber Lulu au Gigy Money namwambia ebu kaza kwenye kipaji chako ebu achana na upuuzi, sasa hivi mabinti wanaotaka kuingia kwenye movie au muziki wasije kwa njia walizopitia Amber Lulu na Gigy,”.

Pia amesema kuwa “Kama 2017 yamefanyika sana, ni serikali au Basata kuja na tamko, hao ni watu wa kutolea tamko atakayeenda kinyume basi sheria ifuate mkondo wake, siyo wakati wakuonyana ni wakati wa tamko kabla ya kuingia 2018,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *