Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amethibitisha kwamba timu hiyo haitoongeza mchezaji mwingine kwa masaa yaliyobaki ya dirisha dogo la usajili baada ya kumsajili Yohana Mkomola pamoja na beki Festo Kayembe kutoka Balende FC ya DRC.
Wachezaji hao walisajiliwa mapema mwezi uliopita baada ya dirisha la usajili kufunguliwa, huku akisema kwamba isingekuwa tatizo la majeruhi ya baadhi ya wachezaji wao muhimu wasinge sajili hadi dirisha kubwa la usajili.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara wanajiandaa na mashindano ya Mapinduzi pamoja na kombe la Shirikisho huku hatua ya 12 ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mpira wa miguu.
”Ni kweli tumefanya baadhi ya usajili tatizo likiwa majeruhi ya mara kwa mara kwa wachezaji wetu muhimu, labda wasingekuwa majeruhi tusinge sajili,” amesema.
Dirisha dogo la usajili linafungwa Desemba 23 saa sita usiku. Wakati watoto wa Jangwani wakimaliza hatua ya usajili bado watani wao wa jadi Simba wanahangaika na beki wa Lipuli Asante Kwasi.