Mwanamfalme wa Uingereza, Prince Harry na mpenzi wake Meghan Markle wameonesha picha zao walizosherehekea kuvalishana pete ya uchumba.
Ndoa ya Harry na Markle inatarajiwa kufungwa May 19, 2018 huko St. George’s Chapel, Windsor Castle nchini Uingereza.
Mwanamfalme huyo, wa tano kwenye msururu wa warithi wa ufalme wa Uingereza atafunga ndoa na Bi Markle ambaye ni mwanamuziki wa Marekani.
Harusi yao itafanyika katika Nottingham Cottage, Kensington Palace jijini London hapo mwakani.
Taarifa kutoka Jumba la Clarence, linaloshughulikia masuala ya Mwanamfalme wa Wales Charles, babake Mwanamfalme Harry na William, imesema maelezo zaidi kuhusu kufanyika kwa harusi hiyo yatatolewa baadaye.