Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amekutana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa ajili ya kujadili masuala ya uchaguzi wa haki nchini baada ya vyama hivyo kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio.

Leo December 21, 2107 Zitto amekutana na Mbowe ikiwa ni siku chache baada ya kutoa taarifa kwamba watavizungukia vyama vyote vya siasa ili kujadilia masuala ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa chama hicho, Abdallah Hamis kikao cha chama hicho kilichoketi hivi karibuni na kuamua kugomea kushiriki uchaguzi wa marudio katika Kata na Majimbo mbalimbali nchini unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.

“Kamati Kuu ya ACT iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, kwa kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani.

“Lengo ni kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vya chama tawala za kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini,”.

Zitto ameanza mazungumzo hayo na Mbowe, wakati Katibu Mkuu wa chama hicho, Dorothy Semu, akiwa anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza suala hilo.

“Nilipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama, jana nimezungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia aliyeko hospitalini KCMC baada ya hapo nimekutana na Mbowe na kujadili kuhusu mazingira ya chaguzi za haki nchini,”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *