Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kusitisha misaada ya kifedha kwa nchi ambazo zinaunga mkono maazimio ya umoja wa mataifa ya kupinga Jerusalem kutambulika kama mji mkuu wa Israel.
Mapema mwezi huu, Bwana Trump alichukua uamuzi huo licha ya kukabiliwa na ukosolewaji mkubwa kutoka mataifa mbalimbali.
Maneno yake hayo yanakuja baada ya Mkutano wa Umoja wa mataifa kupiga kura kupinga hatua yoyote ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Haki miliki ya picha EPA Image caption Mkutano wa Umoja wa mataifa kupinga hatua yoyote ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Muswada wa maazimio haukuitaja Marekani lakini unasema maamuzi yoyote juu ya Jerusalem yanatakiwa kubatilishwa.
Mapema, Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Bi Nikki Haley aliwaonya wanachama wa umoja wa mataifa kuwa Rais Trump amemtaka kuwaripoti wale watakaopiga kura ya kuipinga Marekani.
Mji wa Jerusalem unaobishania una maeneo matakatifu ya dini tatu zenye kufuata imani ya Ibrahim – Uyahudi, Ukristo na Uislamu – sana maeneo mengi yanapatikana Jerusalem Mashariki.
Israel ilitwaa eneo hilo kutoka Jordan wakati wa vita kati ya nchi za Kiarabu na Israel mwaka 1967 na imekuwa ikiuchukulia mji wote kuwa mji wake mkuu ambao hauwezi kugawanywa.
Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa) na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu pamoja na Wapalestina wenyewe.