Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha nchini humo ANC.

Ramposa ambaye alikuwa makamu wa rais wa chama hicho aliweza kumshinda mpinzani wake Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye ni waziri wa zamani na alikuwa mke wa rais Zuma kwa kura 2440 kwa 2161.

Kwa sasa Ramaphosa ameoneka kuwepo kwenye nafasi kubwa ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Hata hivyo Cyril Ramposa amekuwa kiongozi wakati ambao Afrika kusini inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinafanya mambo hayendi sawa katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika .

Cyril Ramposa alizaliwa tarehe 17 mwezi novemba mwaka 1952 mjini Soweto, ndio mwanasiasa tajiri zaidi Afrika Kusini ,utajiri wake unakisiwa kuwa ni dola milioni 450.Tangu ujana wake Ramposa alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa shupavu na hiyo ndio ilimfanya kujiunga na uongozi wa chama cha wafanyakazi .

Na wakati chama cha ANC kilipochukua uongozi wa Afrika kusini mwaka 1994,alitamani sana kuwa naibu wa mwasisi wa Afrika Kusini mpya ,Nelson Mandela lakini pale Mandela alipompuuza na badala yake kumteua Jacob Zuma inasemekana kuwa bwana Ramaphosa alisusia hata sherehe za kuapishwa kwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini vilevile alisusia kuchukua wadhifa wowote wa uongozi katika serikali mpya ya Afrika Kusini.

Badala yake bwana Cyril Ramaphosa ambaye alisomea uwakili alihiari kuwa mbunge na mwenyekiti wa bunge la katiba ambalo lilishughulikia kutengeneza katiba ambayo ilisifiwa sana duniani.

Badaye Ramaphosa alishangaza wengi alipojiuzulu kutoka kwenye siasa na kushughulika zaidi katika biashara zake lakini mwaka 2012 alishawishika tena na kurudi kwenye siasa na kuwa na ilipofika mwaka 2014 alipanda zaidi na kuwa makamu wa rais.

Na wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kurudi kwake Ramaphosa kwenye chama cha ANC kulirudisha imani ya wananchi wengi licha ya kuwa chama hicho kilikuwa kinakabiliwa na kashfa nyingi za kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *