Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetakiwa kuhakikisha inafutata sekta ya ushirika na kuwachukulia hatua kali watendaji wote waliohujumu ushirika na kusababisha machungu kwa wanaushirika ili iwe fundisho kwa wengine.
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza hayo wakati akifungua maadhimisho ya nane nane kwa kanda ya nyanda ya juu kusini yaliyofanyika katika uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Waziri mkuu pia ameitaka wizara hiyo kupitia upya sekta ya ushirika kwa kuanza na viongozi waliopo ndani ya wizara hadi mkoani kuhakikisha kama wanafanya kazi zao upasavyo na kuwaondoa watakaobainika kwa uzembe.
Waziri mkuu amesema kuwa mkulima, mfugaji na mvuvi mdogo au mmoja mmoja hawezi kupunguza umaskini bila ya kuwa na chombo cha kuwaunganisha na kuwapa nguvu ya kuwatetea bei ya mazao yao kama ushirika.
Kwa upande mwingine waziri mkuu, Kassim Majaliwa amesema wizara inatakaiwa kuwahimiza na kuwashawishi wakulima, wafugaji na wavuvi kujinga katika vikundi vya ushiruika vya uzalishaji na SACCOS.
Waziri mkuu amesema kwamba elimu ya ushirika inayotolewa kwenye maonesho mwaka huu iwe changamoto kwa wizara hiyo kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.