Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Dk. John Pombe Magufuli ameendelea kusimamia azma yake ya kumaliza rushwa ndani ya chama hicho.
Dk Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano amesema CCM haitasita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo itabainika rushwa imetumika.
Akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18,2017 Rais Magufuli amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa.
Amewataka wajumbe wa mkutano kuchagua watu waaminifu na wenye mapenzi ya dhati na CCM.
Rais Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho ulioanza Aprili, 2017.