Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amefunguka na kumjibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kauli yake ya kusema kuwa utaratibu uliotumika kumsafirisha Tundu Lissu kwenda Nairobi kuwa ulikwenda kinyume na mfumo wa serikali na kibunge.

Tundu Lissu anadai kuwa kauli hiyo haina ukweli hata kidogo kwani kitendo cha yeye kusafirishwa kwa ndege mnamo Septemba 7, 2017 majira ya usiku kuelekea kwa matibabu nchini Kenya ni wazi kuwa kibali kilitolewa na serikali pamoja na Bunge kwani bila hivyo yeye asingeweza kusafirishwa.

Aidhaa Tundu Lissu aliendelea kufafanua kuwa “Nimesema mimi siombi fadhila, hakuna mtu anaomba kufadhiliwa hapa mimi naomba haki ambayo anatendewa mtu aliye Mbunge anayeumwa ambaye amelazwa nje ya kituo chake cha kazi hicho tu.

Mbali na hilo Tundu Lissu amesikitishwa na upelelezi unaofanywa na jeshi la polisi kuhusu shambulio lake la kutaka kuuawa na kusema anashangaa mpaka leo jeshi la polisi halijasema linamshuku nani kuhusika na shambulio hilo na mpaka leo jeshi la polisi halijaweza kumhoji japo aweze kutoa maelezo yake.

Tundu Lissu alishambuliwa na risasi mnamo Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi kupatiwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo huko kwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *