Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Inspector Haroun amedai kwamba hakuwahi kuwa na bifu na Juma Nature bali bifu hiyo ilitengenezwa na mashabiki.
Inspector amesema kuwa wakati yeye anaoa mwanamke na kuhamia Kijitonyama kutoka Temeke ndio kipindi ambacho Juma Nature na kundi lake la TMK walitoa ngoma ya ‘Shibe shibe’
”Katika mistari ya nyimbo hiyo wamesema ‘nyumbani ni nyumbani’ watu wakawa wanajua kuwa kuhama kwangu Temeke ndio akanitungia nyimbo hiyo, baada ya muda kidogo mimi nimetoa ‘Mishe mishe’ basi ndio tukawachanganya sana kumbe wala haikuwa hivyo mimi na Nature hatuna tatizo tuko pamoja sana”.
Msanii huyo amesema kufanikiwa kwake kulitokana na kushiriki katika shindano la kusaka vipaji lililofanyika Don Bosco, ambapo DJ Bony Love alikuwa Jaji wa shindano hilo, yeye na Luteni Kalama wakaibuka washindi.
Alipoulizwa kuhusu wasanii kutoa nyimbo ambayo haidumu kwa muda mrefu, amesema inatokana na kukosa ubunifu ambapo wakati wao wanang’aa walikuwa wanatumia muda mwingi kuandaa ngoma zao.