Baada ya Kala Jalemiah kusifiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu kutokana na wimbo wake ‘Kijana’, msanii huyo amesema anajipanga kuilipa heshima hiyo aliyopewa.
Kala amesema kuwa amefanya mziki kwa mda mrefu ila ajawahi kupata pongezi kutoka kwa kiongozi mkubwa wa nchi kama tena mbele za maelfu ya watu mara nyingi wamekuwa wakikutana na viongozi wa kawaida na kutupa pongezi za kawaida.
Kala ameongeza kuwa alizipokea salamu za Makamu wa Rais kutoka kwa watu wengi kitendo ambacho amekipokea kwa mikono miwili na kuwa kauli hiyo ya Makamu wa Rais imempa deni la kuendelea kukaza buti na kuandaa nyimbo nyingi zitakazo kuwa mkombozi kwa Jamii.
Pia Kala amesema kauli ya Makamu wa Rais imempa faraja yeye na familia yake kwa ujumla na hata alipotumiwa kile kipande cha video ambayo Makam wa Rais alikuwa anamsifia.
Msanii huyo wa Hip Hop anafunga mwaka kwa kauli yake ya kuwa hakuna mziki wa biashara bali kuna biashara ya muziki.