Kampuni ya Green Telecom Limited leo imezindua kampeni ya ‘Ishikistaa’ season 2 ambapo wananchi watapata fursa ya kukutana na staa anayempenda pamoja na kushinda zawadi mbalimbali.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja kampeni wa Ishikistaa, Beatrice Mbwiga amesema kuwa Ishikistaa ni project inayomuwezesha na kumpa mtu fursa ya kuishi kama staa pamoja na kupata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali atakaposhiriki project hiyo.

“Ishikistaa ni kampeni maalum inayoumuwezesha mtu kuishi kama staa kwa kukutana na staa maarufu wa Bongo anayempenda pamoja na kushinda zawadi mbalimbali”. alisema Beatrice Mbwiga.

Beatrice Mbwiga amesema kuwa Ishikistaa season 2 itahusisha mambo matatu muhimu baada ya leo kuzinduliwa rasmi la kwanza itakuwa Tv series, pili Ishikistaa Night na la mwisho ni Ishikistaa vibe.

Pia meneja project huyo ameongeza kwa kusema kuwa jinsi ya kushiriki project hiyo unatakiwa kutuma STAR kwenda 15670  ambapo utaulizwa maswali na ukishinda utafanikiwa kukutana na staa wako huyo unayempenda pamoja na kushinda trip ya kwenda nchini Afrika Kusini katika mji wa Johannesburg.

Kwa upande wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba Boy ambaye aliwahi kushiriki Ishikistaa season 1 amewataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili kufanikisha ndoto zao za kukutana na wasanii wao wanaowapenda pamoja na kushinda zawaidi kem kem kutoka katika kampeni hiyo.

Naye msanii wa Bongo Fleva, Msamii amesema kuwa ni wakati kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili kufikia ndoto zao kutokana na ushiriki wao kwenye kampeni hiyo iliyozinduliwa leo.

Green Telecom ni kampuni inayojihusisha na masuala ya kuboresha huduma za Tehama na Mawasiliano, pamoja na kutoa huduma za sms kwa ajili ya kuwaunganisha wateja wake mbalimbali na huduma zilizopo sokoni kama vile IVR,USSD,BULK,SHOT CODE NA MOBILE MONEY.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *