Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amewachana baadhi ya watu wanaoisema na kuiponda ndoa yake na Uchebe iliyofungwa wiki iliyopita.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa ya siri wiki iliyopita iliyofanyika Nyumbani kwa Meneja wa Diamond Babu Tale na kuhudhuriwa na watu wasiopungua kumi.

Tangu ndoa hiyo imefungwa kuna maneno mengi yameibuka mitandaoni hasa kwa sababu kuna ripoti zilizodai kuwa familia ya Shilole haikukubaliana na ndoa hiyo hadi kufikia hatua ya ugomvi mkubwa kutokea kati ya Shilole na Dada yake hadi kufikia hatua ya kupelekana polisi.

Baada ya maneno kuzagaa mtandaoni kuhusu Ndoa hiyo Shilole ameibuka na kudai kusikitishwa na habari za majungu zinazoendelea kusambaa kumhusu mume wake Uchebe.

Lakini pia Shilole ameeleza kuwa pamoja na kwamba watu wanamchafua lakini anaamini ndoa yake itadumu na kwa sasa familia yake ipo vizuri na ndoa yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *