Mrembo na Video queen maarufu Bongo, Irene amefunguka na kukiri kuwa miezi michache iliyopita alibeba ujauzito wa Diamond lakini kwa bahati mbaya ujauzito uliharibika.
Irene alijipatia umaarufu zaidi baada ya kutokea kwenye video ya msanii wa WCB Rayvanny kwenye wimbo wake wa kwetu.
Lakini Irene alizidi kujipatia umaarufu pale habari zilipoanza kusambaa kuwa anatembea na msanii maarufu wa Bongo fleva, Diamond Platnumz lakini taarifa hizi zilipata umaarufu zaidi kwa sababu katika kipindi hiki chote Diamond bado alikuwa jwenye uhusiano na mama watoto wake Zari.
Habari za Irene kuwa na mimba ya Diamond zilianza kusikika miezi michache iliyopita lakini kulikuwa hamna uhakika wowote kuwa kama taarifa hizi zina ukweli wowote kwani kuna watu waliodai kuwa mimba ile ilikuwa ya msanii Rayvanny, lakini tetesi hizo zilisimama baada ya mimba hiyo kuacha kuonekana na watu kudhani kuwa ameitoa au alikuwa hana mimba kabisa.
Mrembo huyo alikiri kuwa ni kweli alikuwa mjamzito na Mimba hiyo iliharibika na baba alikuwa Diamond.
Tetesi za Diamond kutoka na mrembo Irene zilizidi kushika hatamu hata pale ishu ya Hamisa ilipobumburuka kwani kuna taarifa mbali mbali zilizoenea mtandaoni kuwa walionekana nchini Afrika Kusini.