Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) limepanga ratiba ya michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika pamoja na kombe la Shirikisho.
Katika ratiba hiyo klabu za Tanzania, Simba na Yanga zimepangwa na wapinzani wao kutoka nchi za Shelisheli na Djibouti.
Yanga ambayo inashiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika imepangiwa na klabu ya St. Louis kutoka visiwa vya Shelisheli huku Simba ambayo inashiriki mashindano ya kombe la Shirikisho imepangiwa kucheza na Gundarmerie Natinal kutoka nchini Djibout.
Timu zote zinatarajia kuanza kucheza mechi zao za kwanza nchini Tanzania huku wakimalizia mechi za mkondo wa pili wakiwa ugenini.
Yanga anashiriki mashindano hayo baada ya kutwaa ubingwa wa ligi Tanzania Bara huku Simba akishiriki mashindano hayo baada ya kutwaa kombe la Shirikisho la Azam.