Baada ya Rais Magufuli kuwaachia huru, Nguza Viking maarufu kama ‘babu Seya’ na mwanawe Jonson Nguza maarufu kama Papii Kocha, Dr. Luis Shika adai ahofii kupoteza kwa kiki yake.
Dk. Shika amesema hamjui wanamuziki hao waliotolewa jela kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika.
Dr. Shika amesema wakati Babu Seya anaingia nchini Tanzania yeye alikuwa nje ya nchi hivyo hajawahi kumuona lakini anafahamu nyimbo zake ambazo aliwahi kuimba.
”Simfahamu Babu Seya, wakati anaingia nchini tayari nilishaondoka nchini muda mrefu, lakini nafahamu nyimbo zake ile aliyoimba baba na mwana tunaimba na kucheza ndio haswa naifahamu vizuri”, amesema.
Pia Dr. Shika amempongeza Rais Magufuli kwa kuwatoa wafungwa mbali mbalimbali na kutumia vizuri fursa ya uongozi kama mkuu wa nchi. ”Nampongeza Rais Magufuli kwa tukio hili la kuwatoa wafungwa na kuwapa uhuru wakaanze maisha yao upya”, ameongeza.
Nguza Viking maarufu kama ”Babu Seya” na Johnson Nguza ”Papii Kocha” walipatikana na hatia ya kubaka na kunajisi watoto na walihukumiwa kwenda jela maisha tangu mwaka 2004 kabla ya kupata msamaha mwaka huu wakiwa wamedumu gerezani kwa miaka 13.