Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Dee ameibuka na kudai kuwa kitendo cha yeye kuiga wimbo wa Mr.Nice Ilikuwa ni kwa sababu ya heshima aliyonayo kwenye mziki wake na wala sio wizi kama anavyodai yeye.

 Baada ya Young Dee kutoa wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Kiben10 ambao ndani yake ameweka kionjo cha wimbo wa Mr.Nice.

 Baada ya Mr. Nice alipousikia wimbo huo alimjia juu Young Dee kwenye mitandao ya kijamii na kudiriki kumuita mwizi wa kazi zake na kutishia kumchukulia hatua za kisheria.

Young Dee amemjibu Mr. Nice na amejitetea kuwa yeye kuimba wimbo wake haikuwa kwa nia mbaya bali alifnya vile kwa sababu alikuwa shabiki Mkubwa wa wimbo wa Mr. Nice.

Lakini hadi sasa Mr Nice ajasema kama atamchukulia sheria gani mwanamuziki huyo baada ya kukopi wimbo wake uliompa umaarufu wa King’asti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *