Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Mwan FA amesema kuwa licha ya kumaliza tofauti zake na Lady Jaydee lakini bado hawajapanga lini watafanya kolabo.

FA amefunguka kauli hiyo baada ya kuonekana pamoja wakiwa studio siku chache baada ya kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda mrefu ambapo kwasasa tofauti hizo zimeisha baada kuonekana pamoja.

Wawili hao walikuwa na tofauti miaka ya nyuma ambapo wamekaa zaidi ya miaka minne kutokuongea baada ya bifu kudumu kwa muda mrefu.

Mwana FA amesema bado ni mapema kusema moja kwa moja kuna kazi inakuja kwani ndio wametoka kumaliza tofauti zao ila kadiri muda unavyozidi kwenda kuna uwezekano wa kufanya tena kazi.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kitu cha kwanza kilikuwa ni kumaliza tofauti zao kama marafiki kwanza halafu vitu vingine vyote vitafuata kama kuna uwezekano wa kufanya.

Lady Jaydee na Mwana FA wameshawahi kutoa nyimbo kama vile Hawajui, Msiache Kuongea, Alikufa kwa Ngoma, Wanaume Kama Mabinti na Sitoamka bila kusahau ngoma walioshirikishwa na Ngwea ‘Sikiliza’ na nyingine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *