Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amemshauri mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni muigizaji Shilole baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake Uchebe.

Shamsa amefunguka na kumsahuri Shilole juu ya maisha ya ndoa aliyoyaanza hivi karibuni baada ya kufunga ndoa wiki iliyopita.

Shilole amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu anaejuliakana kwa jian la Uchebe wiki iliyopita ndoa ambayo ilifanyika kimya kimya na kuhudhuria na ndugu pamoja watu wao wa karibu.

Shamsa Ford  ameamua kumshauri Shiloleh  kutulia katika ndoa yake  na kuachana na sifa za kuwa maarufu kutokana na usanii wake bali atulie ili kuweza kufaidi matunda ya ndoa yake.

Katika ukurasa wake wa instagram Shamsa ameamua kufunguka kuhusu swala ilo na kumpongeza kwa uamuzi aliouchukua Shilole.

Mwisho wa mwaka huu umekuwa mwaka mzuri kwa baadhi ya wasanii ambao wameamua kuachana na ukapela na kujiingiza katika maswala ya familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *