Wanawake watatu wamemtuhumu rais Donald Trump kwamba aliwafanyia ukatili wa kijinisa miaka iliyopita kabla hajawa rais.
Hivyo baraza la Congress kumchunguza Trump kutokana na kashfa hizo zilizoibuliwa na wanawake hao.
Wanawake walioibua kashafa hiyo dhidi ya Rais Trump ni Jessica Leeds, Samantha Holvey, na Rachel Crooks wamesema kuwa rais Trump bila ridhaa yao alikuwa akiwa shika shika,kuwabusu kwa nguvu na ukatili mwingine.Lakini hata hivyo ikulu ya white house imesema kuwa madai ya wanawake hao si ya kweli.
Rachel Crooks katika madai yake dhidi ya kashfa hiyo ya rais Trump,anasema kuwa yeye alilazimishwa kupigwa busu na rais Trump nje ya lift ya majengo ya ghorofa za Trump enzi hizo akiwa na miaka 22. Japo kuwa mkasa huo ulitokea miaka mingi iliyopita,anasema bado Trumpa anapaswa kuchukuliwa hatua.
Mwanamke mwingine anayemtuhumu rais Trump ni mlimbwende wa mwaka 2006 Bi Samantha Holvey ambaye anasema ,Trump alihudhuria mashindano hayo na alikuwa anawakagua mwilini kama vile nyama inavyokaguliwa buchani,na amesema kuwa hana nia ya kumchukulia hatua rais Trump bali anaweka wazi kile alichofanyiwa.
Rais Trump tangu aingie madarakani amekuwa akiandamwa na kashfa mbali mbali zikiwemo za kisiasa na zile zinahusiswa na biashara zake.