Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amefunguka na kuwachana baadhi ya watu wanaomsema kuwa tangu ameanza kuwa maarufu mpaka sasa hivi bado anaishi katika nyumba ya kupanga.
Aunty amejitetea na kusema kuwa anakaa katikati ya mji kjitonyama kwa sababu ni karibu na anakofanya shughuli zake nyinginlakini ana nyumba ya kwake mwenyewe Kigamboni lakini hawezi kwenda kukaa huko kwa sababu ni nje ya mji na ni mabli na nyumbani kwake.
Aunty Ezekile ni mamam wa mtoto mmoja wa kike aliyezaa na mcheza dancer maarufu kutoka katika lebel kubwa nchi ya Wasafi chuni ya bosi wao Diamond Platinumz.
Maneno haya yanakuja baada ya wasanii wengi wakiishi maisha ya juu huku wakiwa hawana sehemu za kukaa zaidi ya kupanga nyumba zenye gharama na baada ya muda wanapopata matatizo wanashindwa pa kujistiri na kuanza kuomba msaada.
Lakini bado watu hawapaswi ku-judge na kuongea maneno bila kuwa na uhakika wa kile wanachokuwa wakikiongea kwa sababu sio kila mtu anapenda kuweka maisha yake hadharani.