Muigizaji wa Bongo movie na mwanasiasa Steve Nyerere amezidi kufunguka tena kuhusiana na kitendo cha Wema Sepetu kurudi tena CCM kutoka Chadema.
Wema Sepetu aliwashtua watu wengi baada ya kutangaza kuwa ana rudi rasmi katika chama chake cha siasaCCM huku akikiita ndio nyumba kwake.
Jambo hilo liliwashtua watu wengi kwa sababu February 24 mwaka 2017 Wema alitangaza rasmi kuwa yeye na Mama yake mzazi wanahamia Chadema rasmi.
Steve Nyerere amefunguka na kudai kuwa Wema kurudi CCM ni kitendo ambacho wazee walishakiongelea:
Kwenye mahojiano aliyofanya siku za karibuni Wema amekiri kuwa kwa sasa anapitia kipindi kigumu sana na kinachomsaidia ni maombi kwa Mungu lakini hajajutia uamuzi wake wa kurudi CCM.