Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amesema anaweza kuwa na mahusiano na Billnass ila siyo Dogo Janja kutokana na urafiki wao kuwa wa karibu zaidi.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kivuruge’ amesema kuwa Bill Nass anamvutia zaidi ya Dogo Janja, hivyo anaweza kumtazama kwa jicho la pili.
Amesema kuwa “Dogo Janja ni rafiki yangu, Dogo Janja hayupo kabisa labda Bill Nass watu wanavyomzungumzia naweza nikakaa mwenye pembeni nikasema ok, labda nikamtazama kwa jicho la pili lakini Dogo Janja siwezi hata nikapoteza muda kumfikiria kwa sababu ni nigger wangu”.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Si kwa kwamba (Dogo Janja) siyo type yangu, ni kijana mwenzangu lakini ni rafiki yangu ambaye najua matatizo yake na yeye anajua ya kwangu tuna-share kiasi kwamba siwezi hata kumfikiria lakini Bill naweza kumfikiria”.
Katika hatua ngingine Nandy ameeleza licha ya kuwepo tetesi nyingi kuwa ana-date na Bill Nass hakuna jambo kama hilo na Bill Nass hajawahi hata kumueleza kuwa anamuhitaji.