Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Timbulo amewataka wasanii wa Bongo kutoa kazi zao kwa lengo la kujitangaza nje ya nchi kuliko kutegemea kolabo na wasanii wa nje kwani muda mwingine hazina faida.
Timbulo amesema kuwa inatakiwa wasanii watoe nyimbo bora ambazo zitavuka kimatiafa na siyo kutegemea kolabo za wasanii wa nje ili kufahamika.
Mwanamuziki huyo ameendelea kusema kuwa wasanii wa nje wanajulikana Tanzania kwa kazi zao bora na siyo kutegemea kolabo kama wasanii wa Bongo wanavyotegemea kolabo ili kupaa kimataifa.
Timbulo ametolea mfano kolabo ya Diamond na Davido kwani kolabo hiyo ilimtangaza zaidi Davido hapa nchini kuliko Diamond nchini Nigeria.
Pia msanii huyo amemtolea mfano mwanamuziki, Alikiba kuwa ameweza kushinda tuzo bila kolabo na msanii wa nje na kueleza hivyo ndivyo inatakiwa kwa wasanii wa Tanzania.