Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia amewataka wananchi wa wilaya ya Kinondoni kuchagua Mbunge wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi ujao ili kuharakisha maendeleo katika jimbo.

Mtulia ambaye jana alitangaza kujivua uanachama wa CUF na nafasi zake zote za uongozi ndani ya Chama hicho amesema wananchi endapo watamchagua Mbunge kutoka Chama tawala basi maendeleo yatakuja kwa haraka kuliko Mbunge anayetoka vyama vya upinzani.

Kwa upande mwingine Mtulia amesema yupo tayari kujiunga na CCM na kueleza kuwa hata sababu zilizomfanya ajivue uanachama CUF ni kutokana na utendaji kazi wa Rais Magufuli wa kupambana na rushwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *