Mama mzazi wa msanii Wema Sepetu, Mariam Sepetu amesema kitendo cha Wema kurudi CCM bila kumuomba ushauri ni kitu ambacho kimemdhalilisha kama mzazi.

Mama Wema ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia kitendo cha Mawanaye kurudi CCM, huku lawama nyingi zikiwa zinamuelekea yeye kama mzazi kwa kutomshauri vema binti yake.

Mama Wema amesema watu wanaomshauri Wema kama wazazi wake si watu wazuri akimtaja Steve Nyerere, huku akisema hawana mapenzi ya kweli na Wema kwani alipopata matatizo walimkimbia, na badala yake CHADEMA ndio waliokuwa wakihangaika naye.

Pamoja na hayo mama Wema amesema Wema atabaki kuwa mtoto wake na hawezi kumchukia kwa sababu ya kuhama chama, ingawa kitendo hiko kimemuumiza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *