Mwanasheria maarufu nchini, Albert Msando amefunguka kuhusu video yake akiwa na mwanamuziki Gigy Money iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii mwezi Mei mwaka huu.

Video hiyo ilimuonyesha Msando na Gigy Money wakiwa ndani ya gari, huku Msando akipitisha mkono wake juu ya mwili wa Gigy, wakati huo Gigy Money akikata kiuno huku anacheza muziki.

Amesema kuwa Ile ni moja kati ya sehemu zilizonisaidia katika maisha yangu, ilinisaidia kujua jamii inanichukuliaje na nini inategemea kutoka kwangu. Video ile haikutengenezwa kwa sababu zozote, mimi sikuwa namfahamu Giggy.

Hata hivyo, baada ya video hiyo kusambaa watu mbalimbali walionyesha kuchukizwa na wanavyomfahamu Mwanasheria Albert Msando mtu wanayemwona ana  heshima kubwa na umaarufu katika jamii,  ambapo aliomba msamaha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kuhusu kuacha kusimamia kesi ya wema Msando Amesema “Niliacha kuwa Wakili wa Wema Sepetu baada ya Kibatala na Lissu kuanza kumtetea, bado ni mshikaji wangu, na nimekua nikiona hiyo habari inayozunguka kuhusu Wema Sepetu kujiandaa kurudi CCM, namkaribisha”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *