Baada ya kuachia wimbo mpya ‘Nakaza Roho’ uliogusa maisha yake, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ferooz amesema kuwa alichoimba kwenye wimbo huo ni ukweli mtupu.
Kwenye wimbo huo, Ferooz amegusia kutengwa na watu wake wa karibu ambao walikuwa naye kipindi hiko yupo juu kwenye muziki kutokana na vibao vyake kama vile ‘Starehe’ na nyingine kibao.
Baadhi ya watu wa karibu aliowataja kuwa wamempa kisogo baada ya kufulia ni mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro, Profesa Jay pamoja na mwanamuziki mwenzake Chege.
Ferooz aliyekuwa memba wa Daz Nundaz amesema kuwa watu wake wa karibu wengi wao walimtenga na kumuweka pembeni na kudai hata alipojitahidi kuwatafuta lakini mawasiliano hayakuwa mazuri.
Kutokana na hali hiyo mwanamuziki huyo amesema kuwa hakutegemea kama jamaa zake hao wangemtenga kutokana na namna alivyokuwa akiishi na watu hao.
Pia Ferooz amesema katika kipindi ambacho aliyumba kimaisha alizidi kukatisha tamaa na watu wengi mbalimbali lakini alijipa matumaini na kupigana jambo ambalo anaona limeanza kuleta matumaini kutokana na watu kumpokea vyema na wimbo wake huo mpya ‘Nakaza roho’.