Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Dee amesema kuwa hapendi kushindanishwa na msanii yeyote katika maisha yake binafsi labda kwenye muziki tu.

Young Dee amesema kuwa kushindanishwa ambako ni sahihi ni katika muziki tu na si vinginevyo kutokana huko ndiyo kila kitu kipo wazi lakini kwenye maisha binafsi si mahali pake.

Msanii huyo amesema kuwa mashabiki kuwashindanisha wasanii ni kazi yao kama wao lakini huwa anapenda sana mashabiki wanapokuwa wanashindanisha kazi kwa sababu ndio kitu kinachowakutanisha wasanii nchini.

Ameongeza kwa kusema kuwa nje ya muziki hapendi kushindanisha sehemu nyingine haswa kwenye maisha binafsi kwani kila mmoja ana aina yake ya maisha anayoishi.

Mashabiki wamekuwa wakipenda kuwashindanisha/kuwafananisha Young Dee, Dogo Janja na Young Killer ambao umri wao unafanana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *