Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameingilia kati suala ambalo sasa limeigusa dunia nzima kwa kitendo cha raia wa Libya kuwauza kama watumwa wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Rais Buhari amesema vitendo hivyo havikubaliki, na kwamba wako tayari kufanya lolote kuwalinda raia wake ambao pia ni miongoni mwa wahanga wa biashara hiyo, yenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

“Hali ya Libya ya watu kuuzwa ni ya kutisha na haikubaliki, tutafanya kila kitu kuwalinda raia wetu popote walipo, na pia tumeshaanza kuwarudisha nyumbani wanigeria wote waliopo Libya na sehemu nyingine, tutahakikisha wote wanarejea nyumbani salama na kuhudumiwa”,.

Kitendo cha raia wa Libya kuwauza wahamiaji wanaoingia nchini humo ambao wengi wao ni raia wa mataifa ya Afrika Magharibi, kimeishtua dunia nzima ambapo mpaka watu maarufu mbali mbali duniani, wamekuwa wakipost kwenye mitandao ya kijamii kukemea vitendo hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *