Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wengi wa Tanzania wana uwelewa mdogo sana kwenye suala la mikataba ya kazi.
Msanii huyo amesema kitu hicho kimefanya wawekezaji wengi wakubwa kukimbia katika tasnia ya muziki kutokana na tabia ya wasanii kupenda kuhama label bila kuzingatia sheria za mikataba.
Dudu Baya amesema kuwa “Soko la kumsaini mtu hapa Tanzania ni gumu sana kwa sababu wasanii wa Tanzania ni wajinga sana kwenye mikataba ndio maana hakuna taifa ambalo huwanachoka kwenye tv na redio kusikia fulani amehama label hii, mara nimehama label hii, akikaa kule mwaka mmoja anasema ameibiwa anahamia label nyingine”.
Amesema kuwa “Lakini hawa watu wanaomiliki hizi label ni wavumilivu sana kwa sababu anaangali huyu msanii kakimbia kwenye label mkataba haujaisha anaenda kwenye label nyingine, huyu mtu akienda mahakamani anapoteza muda wake kwa sababu yule msani hata hela ya kumlipa hana”.
Pia amesema kuwa kutokana na tabia hiyo ya wasanii ndio sababu label kama Tetemesha Entertainment, Bongo Records na MJ Records kuacha kusimamia wasanii kutokana na tabia za wasanii hao.