Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Sister P amefunguka na kusema kuwa katika ujio wake mpya kwenye muziki anatamani kufanya kazi na mwanamuziki Alikiba kwani anaamini watafanya kazi kubwa.
Sister P amedai kuwa akifanya kazi na Alikiba lazima itakuwa kazi kubwa na bora zaidi sababu watakuwa wamekutana wanamuziki na si wasanii.
Pia amesema kuwa kiu yake kubwa kufanya kazi moja na Alikiba kwani anaamini itakuwa kazi kubwa zaidi sababu watakuwa wamekutana wanamuziki na siyo wasanii.
Sister P ambaye hivi sasa muonekano wake umebadilika tofauti na zamani ameahidi kuwashangaza Watanzania kwa kazi zake mpya na kusema anaamini kuwa atarudi kwenye nafasi yake licha ya kukaa kimya kitambo kwenye muziki.
Mwanamuziki huyo alitamba miaka ya nyuma na ngoma kama vile Anakuja, Hey Dj ambazo zilikonga nyoyo za mashabiki.