Mama mzazi wa Wema Sepetu ameenda jijini Nairobi nchini Kenya kumjulia hali mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye anapata matibabu baada ya kushambuliwa na risasi.
Mama Wema ameenda Nairobi ikiwa ni mwezi wa pili toka Tundu Lissu ahambuliwe kwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma ambapo alipigwa risasi zaidi 38.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa akitibiwa Nairobi tangu aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi September mwaka huu.
Viongozi mbali mbali wa kiserikali na wa chama hicho wamekuwa wakienda kumjulia hali ambapo jana makamu wa Rais Samia Suluhu alikwenda kumtembelea kiongozi huyo.