Mkoa wa Mwanza umezindua mwongozo wa uwekezaji ukiweka mikakati ya kuupiku Dar es Salaam katika uchangiaji wa pato la Taifa.

Mwongozo huo umeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema jana kuwa fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya kilimo, uvuvi, madini, viwanda na biashara ndizo zitatumika kuipiku Dar es Salaam.

Mtaalamu kutoka ESRF, Dk Bohela Lunogelo amesema pato la mwananchi wa Mkoa wa Mwanza ni zaidi ya Sh2 milioni kwa mwaka.

Mongella amesema mkoa utaunda timu maalumu ya wataalam kutoka mamlaka, taasisi na idara za Serikali zinazohusika na utoaji wa vibali na leseni ili kuwapunguzia wawekezaji urasimu wa kimfumo, hasa vibali na leseni za kuanzisha biashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *