Rais Kenyatta wa Kenya leo ameapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa awamu ya pili baada ya kushinda uchaguzi ulipita.
Kiapo hicho kimefanyika kituo cha Kimataifa cha Michezo Moi, Kasarani jijini Nairobi, kuanzia saa nne asubuhi.
Kiapo hicho kimeongozwa na Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi na kushuhudiwa na Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na wageni 100,000 wa ndani na nje ya Kenya, zitagharimu shilingi milioni 300 za Kenya.).
Baada ya kiapo, jeshi limepiga mizinga 21 kumkaribisha Rais mpya wa nchi hiyo baada ya uchaguzi huliopita na Kenyatta kuibuka mshindi.
Kenyatta amemwalika mpinzani wake mkuu kwenye uchaguzi uliopita, kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani (NASA), Raila Odinga lakini akuhudhuria sherehe hiyo.