Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa Serikali itaanza kutoa hatimiliki za viwanja kati ya siku moja na siku saba kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ifikapo Juni 1, 2018.

Masema hayo leo wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi.

Ameongeza kuwa mfumo huo utaondoa udanganyifu katika kutoa hati kwa watu wawili au zaidi katika kiwanja kimoja na kuondoa migogoro ya viwanja ambayo imekuwa kero kwa wananchi.

Lukuvi amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuondoa utapeli uliokuwa ukifanyika kuhusu ardhi na ndio maana imeanzisha mfumo huo ambao ameuita muarobaini wa migogoro ya ardhi.

Aidha, Waziri Lukuvi alisema kuwa hati ya kisasa itakuwa na ukurasa mmoja badala ya zamani ambayo ilikuwa na kurasa zaidi ya ishirini.

Kwa mfumo huo, maafisa ardhi hawatatumia tena karatasi bali watakuwa na kompyuta ambamo taarifa zote zitahifadhiwa, aliongeza Lukuvi.

Lukuvi amesema kuwa mfumo utaiwezesha Serikali kuwafahamu wamiliki wote wa viwanja na kuwakumbusha muda wa kulipia viwanja vyao, hivyo mapato ya Serikali yataongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *