Muigizaji wa Bongo movie, Wema Sepetu amefunguka na kudai kuwa yeye ndio muigizaji wa Bongo movie aliyeirudishia heshima tasnia ya Bongo movie iliyopotea tangu kifo cha Kanumba.

Marehemu Steven Kanumba alikuwa mmoja wa wasanii wa Bongo movie aliyepata jina na hadhi kwa kuwa msanii aliyejaribu au kuthubutu kuipeleka sanaa ya Bongo movie mbali zaidi. Kanumba alithubutu kuifikisha Bongo movie nje ya Tanzania kwani alicheza filamu na wasanii mbali mbali kutoka nchi mbali mbali kama vile Nigeria.

Tangu kifo cha Kanumba miaka mitano iliyopita sanaa ya Bongo movie imeshuka kwa kiasi kikubwa viwango vya filamu hizo zimeshuka na kupelekea kupoteza soko lake kwani wanunuzi wa kazi hizi hawaoni ubora hivyo wameacha kuzinunua wala kufatilia.

Wema Sepetu alisafiri wiki hii iliyoisha kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya kazi zake kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio Wema alifunguka yafuatayo kuhusiana na  tasnia ya Bongo movie.

Pia Wema alifunguka kuhusu jitihada alizofanya kuirudishia heshima sanaa ya Bongo movie kutokana na movie zake alizofanya hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *