Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa kiwango cha kiungo wake Henrikh Mkhitaryan kimeshuka.

Mkhitaryan, ambaye alijiunga na United kutoka Dortmund mwezi Julai 2016 kwa dau la £26.3m, hakushirikishwa katika kikosi cha United katika mechi mbili zilizopita na jana ndiyo amecheza dhidi ya Brighton ambapo ametokea benchi.

Mourinho alisema kuwa kiwango cha mchezo wa Mkhitaryan kimekuwa kikipungua hatua baada ya hatua

Mkhitaryan alianzishwa mechi 10 kati ya 11 za ligi ya Uingereza kabla ya kuachwa nje baada ya kutolewa katika dakika 62 katika mechi ambayo United ilipoteza kwa Chelsea kwa 1-0 mnamo tarehe 5 mwezi Novemba.

“Sikufurahia kiwango chake cha mchezo”, alisema Mourinho kuhusu mchezaji ambaye amefunga mabao mawili pekee katika mechi 16 alizochezeshwa msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *