Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na hospitali ya BLK ya New Delhi, India imefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria wa upandikizaji wa figo.

Waziri Ummy amesema kwamba upasuaji huo nib juhudi za serikali kuokoa fedha ambazo zingelipwa nje ya nchi kugharamia matibabu hayo na badala yake fedha hizo zitumike kuleta maendeleo kwenye maeneo mengine yenye uhitaji nchini.

Aidha Waziri Ummy amesema kwamba kwa zaidi ya mwaka Hospitali ya Taifa ilijikita kuwekeza kwenye kuongeza ujuzi wa wataalamu wa aina mbalimbali  wakiwemo wa upasuaji wa kupandikiza figo  na kwamba wataalamu 19 walipelekwa nchini India, na Norway kwa ajili ya utaalam,u wa mafunzo hayo.

Pia imeelezwa kwamba utayarishaji wa mgonjwa kwa ajili ya matibabu ya upandikizaji figo ikiwemo vipimo mbalimbali vinavyohitajika kwa mpokeaji figo na mtoaji unagharimu takribani milioni 21 kiasi ambacho ni cha chini tofauti na hapo awali ambapo serikali ilikuwa ikigharamia milion 80-100 kwa mgonjwa mmoja huku ikidaiwa kwa mwaka walikuwa wanasafirishwa wagonjwa hadi 35.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *