Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba amemuonya mama mzazi wa Wema Sepetu baada ya mtoto wake huyo kutohudhuria mahakamani kwaajili ya kuhudhuria katika kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Wakili wa Serikali Agustino Michael ambaye ni Wakili wa serikali aliitaja kesi hiyo mbele ya hakimu Simba kuwa ndiyo iliyokuwa ikitakiwa kuendelea.
Mama huyo ameiambia mahakama kuwa mwanae ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa kuwa amefiwa na shangazi yake hivyo ameenda kushughulikia shughuli za mazishi ndiyo maana hajafika na mimi nimekuja kumuwakilisha.
Baada ya mama huyo kutoa hudhuru huo, Hakimu alimuuliza kama Wema amepatwa na msiba uliomfanya ashindwe kufika mahakamani imekuwaje yeye mama huyo apate muda huo yeye ashindwe?
Hakimu alimueleza mama huyo na kumuambia asichukulie masihara suala la mshtakiwa kuripoti Mahakamani hapo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Disemba 14 mwaka huu itakaposikilizwa tena baada ya kuhairishwa leo.