Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ameapishwa kushika wadifa huo baada ya kujiuzuru kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe aliyedumu kwa miaka 37.

Bw. Emmerson Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Mzee Robert Mugabe kwenye sherehe iliyofanyika katika uwanja wa wa mpira wa taifa hilo jijini Harare.

Mnangagwa kwenye utawala wa Mugabe alihudumu nafasi ya makamu wa Rais na mapema mwezi septemba mwaka huu kufutwa kazi na Mugabe.

Kufutwa kwake kazi kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang’atuke madarakani.

Wananchi wa taifa hilo wana imani na Rais huyo kutokana na utendaji kazi wake katika Serikali ya nchii hiyo wakati akiwa makamo wa Rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *