Aliyetaka kununua nyumba za Lugumi, Dkt. Louis Shika ametunukiwa heshima ya kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya Chuo cha Sayansi ya Dawa  kilichoko Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga,  ambako amepokelewa kama mfalme.

Mapokezi hayo ya kipekee yameanzia uwanja wa ndege wa mjini Kahama alipowekwa kwenye gari la wazi huku msafara mkubwa uliokuwepo ukijumuisha na bodaboda,  magari na mamia ya watu mbalimbali waliojitokeza kumwoma na kumlaki.

Ziara hiyo ya Dkt. Shika mkoani humo itamalizika jioni hii chuoni hapo ambapo anatarajiwa kurejea kwa ndege Dar es Salaam usiku.

Dk Shika amepata umaarufu baada ya kutaka kununu nyumba za Lugumu zilizokuwa zinapigwa mnada jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *