Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ametaja kikosi cha wachezaji 11 ambao ni bora kwa upande wake tangu mwaka 2000 huku akiwatosa nyota wengi wanaocheza ligi kuu kwa sasa.

Kikosi hicho ambacho kina nyota kadhaa waliostaafu kinaundwa na kipa Juma Kaseja, mabeki Shadrack Nsajigwa, Victor Costa, Boniface Pawasa na Ramadhani Wasso.

Katika eneo la kiungo Manara amewataja Athmani Idd ‘Chuji’, Shekhan Rashid na Haruna Moshi ‘Boban’ huku safu ya ushambuliaji ikiwa na Mbwana Samatta, Simon Msuva na Mrisho Ngassa.

Katika kikosi hicho ni wachezaji wawili tu (Kaseja na Ngassa) ndio wanaoendelea kucheza ligi kuu ya Vodacom (VPL).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *