Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda leo ametembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole baada ya ofisi hizo kuungua moto jana.

Jengo la Clouds Media jana limewaka moto majira ya asubuhi lakini ulifnikwa kuzimwa na vikosi vya uokoaji vya jeshi la kuzima moto.

Makonda amefika Ofisini hapo kutoa pole kwa janga la moto lililoipata Ofisi hiyo siku ya jana majira ya saa nne asubuhi.

Viongozi wengine wa serikali waliofika ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Ally Hapi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta.

 Matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV yamerejea hewani baada ya kupotea siku nzima  jana kutokana na hitilafu ya iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *