Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amekataa kuzungumza na wandishi wa habari baada ya mechi ya klabu bingwa dhidi ya Apoel ambapo Real Madrid walishinda 6-0.

Ronaldo alipofuatwa na wanahabari baada ya mchezo huo alikataa kuongea hadi pale walipomganda zaidi lakini alisisitiza kuwa hawezi kuongea chochote na hana raha ya kufanya mahojiano na wanahabari.

Hatua ya Ronaldo kugoma kuongea na wanahabari ni matokeo ya habari zilizoripotiwa hivi karibuni kuwa Ronaldo ana ugomvi na nahdha wake Sergio Ramos baada ya Ronaldo kukaririwa akisema Real Madrid haifanyi vizuri kwenye La Liga kwasababu ina wachezaji wengi ambao si wazoefu baada ya kuwauza Alvaro Morata na James Rodriquez kitu ambacho Ramos alikipinga kwa nguvu.

Baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 6-0 sasa Ronaldo ameifungia Real Madrid mabao 98 kwenye mechi 96, akimzidi mshindani wake Lionel Messi ambaye ameifungia Barcelona mabao 97 kwenye mechi 119.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *