Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Lowassa ambaye ni waziri mkuu mstaafu amesema kuwa amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.
Lowassa amesema kuwa huu ni uongo wa kutunga kwani watu wamekuwa wakitunga vitu dhidi yake ila amesisitiza hana mpango wa kurejea CCM.
Amesema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.
Pia amesema kuwa ni uzushi kuwa watu wamezuiwa kwenda nyumbani kwake kisa Serikali imezuia hivyo.