Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA, Lawrence Masha leo amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuhama Chadema.

Masha amejiunga leo na Chama hicho baada ya kukihama kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mwengine alihmia chama CCM leo ni aliyekuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo, Albert Msando.

Katika hali nyingine ya kushangaza ni kwa Kiongozi mkubwa wa Baraza la vijana wa CHADEMA Taifa, Patrobas Katambi naye ametangaza kuachana na CHADEMA na kujiunga rasmi CCM.

Chama Cha Mapinduzi kinaendelea na vikao vyake vinavyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo vimeanza toka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *