Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne wiki ijayo kuwa Rais kwa muhula wa pili.
Kenyatta ataapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo baada ya Mahakama ya Juu kufutilia mbali kesi ambazo zilikuwa zinapinga ushindi wake katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba.
Kifungu 141(1b) cha Katiba ya Kenya kinasema Rais anafaa kuapishwa siku ya saba inayofuata siku ya kutolewa kwa uamuzi wa mahakama wa kuidhinisha uchaguzi iwapo kulikuwa na kesi iliyokuwa imewasilishwa.
Rais kwa mujibu wa katiba ya Kenya anafaa kuapishwa hadharani mbele ya Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu.